Coca‑Cola nchini Afrika Kusini inaendelea kuwapa watumiaji chaguo kutoka kwenye orodha yake ya vinywaji

19-10-2022

Ikiwa na vinywaji saba vya baridi vyenye kaboni na vyenye kalori chache/kilojuli ya chini kwenye maduka yake, Kampuni ya Coca‑Cola (TCCC), inaendelea kuwapa wateja chaguo licha ya mabadiliko ya hivi karibuni kwenye orodha ya bidhaa zake.

Miaka miwili iliyopita, TCCC ilitangaza kuwa itaaondoa bidhaa fulani katika masoko mbalimbali duniani kote kama sehemu ya uboreshaji wa orodha ya bidhaa yake.

Kwa mujibu wa Silke Bucker, Mkurugenzi Mtendaji wa Masoko wa Coca‑Cola nchini Afrika Kusini, orodha hii ya bidhaa ndio kubwa zaidi kuwahi kutolewa na kampuni ya vinywaji nchini na huwaonyesha watumiaji kuwa uboreshaji wa orodha ya bidhaa ya kampuni hii uliotangazwa mwaka 2020 uliendeshwa na shaukuhamuu ya kutaka kuendelea kukidhi mahitaji ya watumiaji. 

Kwa mujibu wa Bucker: "Uboreshaji huu haukulenga kupunguza orodha ya bidhaa ya TCCC bali ilihusu kutumia mbinu inayotoa kipaumbela kwa watumiaji kwa kuendelea kuzingatia mapendeleo yao ambayo ilisababisha kubadilishwa kwa mkondo wa uwekezaji". 

"Nguvu za bidhaa zetu zenye kalori ya chini au kilojuli ya chini inathibitisha kwamba uboreshaji unakidhi lengo la kutoa kipaumbele kwa watumiaji wetu," alisema.

Kama sehemu ya uboreshaji, TCCC ilitangaza kuwa itasitisha TaB® duniani kote, ikiwa ni pamoja na Afrika Kusini. Hata hivyo, kampuni ambayo ilianzisha aina hiyo ya kinywaji lishe mwanzoni mwa miaka ya 1990, inaendelea kuwa mtangulizi katika kitengo hicho ili kuwapa watumiaji nafasi za kuchagua vinywaji vyenye kalori chache au kilojuli ya chini ambavyo haviwezi kulinganishwa na vingine.

Aina nne ya vinywaji hivyo vinauzwa chini ya chapa ya Coca‑Cola®, ambayo ilichaguliwa kama ''kinywaji baridi cha kifahari'' nchini Afrika Kusini kulingana na Utafiti wa 2021 wa Sunday Times GenNext. 

Aina hizo nne ni Coca‑Cola® No Sugar, Coca‑Cola® Light, Coca‑Cola® Original Taste, na Coca‑Cola® No Sugar No Caffeine. Zingine ni Fanta® No Sugar, Sprite® No Sugar, na Stoney® Ginger Beer No Sugar. 

“Tunashukuru TaB kwa kutengeneza njia kwa ajili ya bidhaa zetu zenye kalori ndogo au kilojuli ya chini, na kwa kikundi cha wale wanaopenda TaB ambao wamekubali brandi hiyo kwa karibu miongo sita. Iliyojumuiswa kwenye orodha ya bidhaa hizo ni Coca‑Cola No Sugar No Caffeine. Kwa kiasi kikubwa inazingatiwa kuwa mrithi wa chapa ya TaB, hakika inatoa manufaa sawa ya bidhaa bila kuathiri ladha na ubora,” alihitimisha Bucker.

Uboreshaji huo wa bidhaa kote duniani umetoa changamoto kwa TCCC kufikiria kwa njia tofauti kuhusu chapa zake ili kuharakisha mikakati ya kubadilika na kuwa kampuni ya vinywaji vya aina mbalimbali. Bidhaa mpya kama vile Coca‑Cola No Sugar No Caffeine ni sehemu ya juhudi za kampuni kufahamisha watumiaji kuhusu bidhaa mbalimbali na kuwapa uhuru na uwezo wa kuchagua wanapotumia bidhaa hizo.

Ili kudumisha muhimu, TCCC itaendelea kusikiliza na kujibu mahitaji ya watumiaji kwa kuwapa watumiaji vinywaji wanavyotaka.