Watu ni Muhimu

Tunaamini kuwa mazingira ya kazi yenye utofauti, usawa na jumuishi yanatufanya tuwe na nguvu zaidi kama kampuni, yanatuwezesha kuunda mustakabali bora kwa wafanyakazi na jamii, husaidia upatikanaji wa fursa sawa na hujenga hisia ya kujiona sehemu ya maeneo yetu ya kazi na katika jamii.

Mbali na wafanyakazi wetu wenyewe, tunafanya kazi na mamia ya washirika, maelfu ya wauzaji na mamilioni ya wakulima duniani kote. Lengo letu ni kusaidia kuendeleza jamii zinazostawi na zinazostahimili kama sehemu ya utaratibu wa uzalishaji na uuzaji wa bidhaa ulio salama na wa kudumu kwa muda mrefu.

Tunachukua hatua za kujenga maisha bora ya baadaye kwa kuwekeza katika uwezeshaji wa kiuchumi, utofauti, usawa na jumuishi; na kutoa misaada kupitia Wakfu wa Coca‑Cola.

Sehemu za Jamii Tunazozipa Mkazo

Malengo ya Maendeleo Endelevu ya Kimataifa, Mipango na Hatua Zilizopigwa

Ripoti ya 2021 ya Mazingira, Jamii na Utawala wa Biashara

Tunatengeneza chapa na bidhaa zinazopendwa na watu huku tukijenga mustakabali endelevu kwa ajili ya biashara na sayari yetu. Tunafanya yote hayo huku tukisalia waaminifu kwa madhumuni yetu: kuburudisha ulimwengu na kuleta mabadiliko.

Kituo cha Nyenzo Endelevu

Nyenzo hii inatoa muhtasari wa juhudi zetu za kuunda biashara endelevu zaidi na maisha bora ya ushirikiano katika siku zijazo na inayoleta mabadiliko katika maisha ya jamii na sayari yetu.