Je, kafeini katika Coca‐Cola huleta uraibu?

Kafeini ni kichocheo cha kiwango cha chini, na ikiwa unainywa mara kwa mara na kisha kuacha ghafla, unaweza kupata maumivu ya kichwa au athari zingine ndogo. Lakini wengi wetu tunaweza kupunguza au kuondoa kabisa kafeini katika lishe zetu bila matatizo makubwa.

Watu wengi ulimwenguni hufurahia kunywa kafeini kila siku, katika vinywaji kama kahawa, chai na vinywaji baridi. Mara nyingi watu hushangaa wanapogundua kuwa Coca‐Cola ina kafeini kidogo sana kuliko kiasi kile kile cha kahawa.

Tunajua kwamba si kila mtu hunywa kafeini na si kila mtu anataka kuinywa kila wakati. Pia tunatoa aina mbalimbali za vinywaji visivyo na kafeini ili watu waweze kujichagulia wenyewe na pia kuzichagulia familia zao.

Je, ulikua unajua? Tuna aina mbalimbali ya vinywaji baridi vilivyotengenezwa bila kafeini, kama vile Caffeine-Free Diet Coke, Sprite, Lilt na Fanta.