Maswali Yanayoulizwa Mara kwa Mara | Coca‑Cola Afrika Kusini

Chagua kategoria ili kutumia kichujio 

Kiburudisho kipya kinachofanya Coca‑Cola Zero Sugar kuwa na ladha sawa na ile ya Coca‑Cola asili (Coca‑Cola Classic) ila haina sukari.

 

Jina jipya – Coca‑Cola Zero Sugar – ili kueleza wazi zaidi kuwa kinywaji hakina sukari.

Muonekano mpya – Njia mpya ya kupakia ili kuonyesha mkakati wetu wa kimataifa wa chapa moja na kupanua mvuto wa kifahari wa chapa ya Coca‐Cola na diski nyekundu kwa toleo la Coca‑Cola lisio na sukari. 

Inafanana sana na Coca‑Cola Original.

Iwe unakunywa ya kwenye kopo au ya kwenye chupa, Coca‐Cola ni ile ile siku zote. Ni mapishi yale yale, viambato vile vile na mchakato sawa wa utengenezaji kila wakati.

Je, ulikua unajua? Mtazamo wako wa ladha unaweza kuathiriwa na mambo mengi, kama vile jinsi Coca‑Cola ilivyo baridi au ikiwa unakunywa moja kwa moja kutoka kwenye kopo au kuimimina kwenye glasi.

Kuna miligramu 33 katika kopo la mililita 330 za Coca‑Cola. Mara nyingi watu hushangaa wanapojua kwamba kopo la Coca‐Cola lina kafeini kidogo sana kuliko kiasi kilekile cha kahawa.

Kila siku, mamilioni ya watu hufurahia vinywaji vilivyo na kafeini ikiwa ni pamoja na kahawa, chai na vinywaji baridi. Kwa sababu kafeini imekuwa ikitumika kwa karne nyingi, tunafahamu mengi kuhusu kafeini– imetafitiwa sana na inajulikana kuwa salama katika viwango vinavyotumika kwenye vinywaji vyetu.

Tunafahamu kuwa si kila mtu hunywa kafeini na si kila mtu anataka kuinywa kila wakati, hivyo tuna aina mbalimbali za vinywaji visivyokuwa na kafeini, ikiwa ni pamoja na TAB ili watu waweze kujichagulia wenyewe na pia kuzichagulia familia zao.

Kiungo cha kuongeza ladha ya utamu na kisicho na sukari ya kawaida kinachopatikana maliasili.

Majani ya stevia yana chanzo cha kipekee cha utamu wa asili. Hayana kalori. Mmea wenyewe ni wa familia ya chrysanthemum, mmea wenye asili ya Kiasia. Tunatumia dondoo ya mmea wa stevia kupunguza sukari na kalori katika baadhi ya vinywaji vyetu kama vile Sprite, glaceau vitaminwater na Coca‐Cola Life.

Je, ulikua unajua? Stevia imetumika Amerika Kusini kuongeza ladha kwenye vinywaji kwa zaidi ya miaka 200.

Kiungo cha kuongeza utamu kilicho na kalori chache.

Tunatumia aspartame pamoja na kiungo kingine chenye kalori chache, acesulfame-K, ili kuongeza ladha ya utamu kwenye baadhi ya vinywaji vyetu.

Je, ulikua unajua? Aspartame ina utamu wa zaidi ya mara 200 ikilinganishwa na sukari ya kawaida.

Hapana.

Viambato na mchakato wetu wa utengenezaji unadhibitiwa vikali na serikali na mamlaka za afya katika nchi zaidi ya 200. Wote wameitambua Coca‑Cola kama kinywaji kisicho na vileo. 

Je, ulikua unajua? Coca‑Cola ni kampuni kubwa zaidi ulimwenguni ya vinywaji visivyo na vileo.

Wagonjwa wa kisukari wanaweza kunywa Coca Cola Light/ Zero; hata hivyo, tunapendekeza uwasiliane na daktari wako kuhusu kisukari na mahitaji yako ya lishe.

Kafeini ni kichocheo cha kiwango cha chini, na ikiwa unainywa mara kwa mara na kisha kuacha ghafla, unaweza kupata maumivu ya kichwa au athari zingine ndogo. Lakini wengi wetu tunaweza kupunguza au kuondoa kabisa kafeini katika lishe zetu bila matatizo makubwa.

Watu wengi ulimwenguni hufurahia kunywa kafeini kila siku, katika vinywaji kama kahawa, chai na vinywaji baridi. Mara nyingi watu hushangaa wanapogundua kuwa Coca‐Cola ina kafeini kidogo sana kuliko kiasi kile kile cha kahawa.

Tunajua kwamba si kila mtu hunywa kafeini na si kila mtu anataka kuinywa kila wakati. Pia tunatoa aina mbalimbali za vinywaji visivyo na kafeini ili watu waweze kujichagulia wenyewe na pia kuzichagulia familia zao.

Je, ulikua unajua? Tuna aina mbalimbali ya vinywaji baridi vilivyotengenezwa bila kafeini, kama vile Caffeine-Free Diet Coke, Sprite, Lilt na Fanta.

Ndiyo. Shirika la Viwango vya Chakula linapendekeza kwamba wanawake wajawazito hawapaswi kunywa zaidi ya miligramu 200 ya kafeini kwa siku. Kopo la Coca‐Cola Classic lina miligramu 32 ya kafeini na kopo la Diet Coke lina miligramu 42.

Je, ulikua unajua? Tuna vinywaji mbalimbali visivyo na kafeini ikiwa ni pamoja na Caffeine-Free Diet Coke, Oasis, Fanta, Lilt, Sprite, 5 Alive na bila shaka, glacéau smartwater.

Bado una maswali?