Ni kiasi gani cha kafeini kilicho katika Coca‐Cola?
Kuna miligramu 33 katika kopo la mililita 330 za Coca‑Cola. Mara nyingi watu hushangaa wanapojua kwamba kopo la Coca‐Cola lina kafeini kidogo sana kuliko kiasi kilekile cha kahawa.
Kila siku, mamilioni ya watu hufurahia vinywaji vilivyo na kafeini ikiwa ni pamoja na kahawa, chai na vinywaji baridi. Kwa sababu kafeini imekuwa ikitumika kwa karne nyingi, tunafahamu mengi kuhusu kafeini– imetafitiwa sana na inajulikana kuwa salama katika viwango vinavyotumika kwenye vinywaji vyetu.
Tunafahamu kuwa si kila mtu hunywa kafeini na si kila mtu anataka kuinywa kila wakati, hivyo tuna aina mbalimbali za vinywaji visivyokuwa na kafeini, ikiwa ni pamoja na TAB ili watu waweze kujichagulia wenyewe na pia kuzichagulia familia zao.