Stevia ni nini?

Kiungo cha kuongeza ladha ya utamu na kisicho na sukari ya kawaida kinachopatikana maliasili.

Majani ya stevia yana chanzo cha kipekee cha utamu wa asili. Hayana kalori. Mmea wenyewe ni wa familia ya chrysanthemum, mmea wenye asili ya Kiasia. Tunatumia dondoo ya mmea wa stevia kupunguza sukari na kalori katika baadhi ya vinywaji vyetu kama vile Sprite, glaceau vitaminwater na Coca‐Cola Life.

Je, ulikua unajua? Stevia imetumika Amerika Kusini kuongeza ladha kwenye vinywaji kwa zaidi ya miaka 200.