Karibu kwenye Sera ya Faragha ya Watumiaji ya Coca‑Cola

Kampuni ya Coca‑Cola pamoja na washirika wake (kwa pamoja, Coca‑Cola au sisi) wanachukua haki yako ya faragha kwa uzito sana. Tunafurahia kwamba unatuamini na maelezo yako ya kibinafsi na kuheshimu faragha yako ni muhimu sana katika mitagusano yetu nawe.

Jinsi Coca‑Cola inavyoshughulikia maelezo ya kibinafsi, inaongozwa na misimamo hii:

  • Uwazi
  • Heshima
  • Uaminifu
  • Haki

Tarehe ya Kuanza Kutumika: 16 July 2024

Sera ya Faragha ya Watumiaji ya Coca‑Cola (Sera ya Faragha) inaelezea maelezo ya kibinafsi ambayo Coca‑Cola hukusanya kutoka kwa watumiaji au kuhusu watumiaji wa tovuti, programu za simu (Programu), wijeti, na huduma nyingine za mtandaoni au za nje ya mtandao zinazoendeshwa na Coca‑Cola (kwa pamoja, Huduma) na jinsi tunavyotumia na kulinda maelezo hayo ya kibinafsi. Sera hii ya Faragha pia inaelezea jinsi watumiaji wanavyoweza kufanya maamuzi kuhusu maelezo yao ya kibinafsi.

Tunapotaja maelezo ya kibinafsi (wakati mwingine tunayataja kama data za kibinafsi chini ya baadhi ya sheria) katika Sera hii ya Faragha, tunamaanisha maelezo yanayomtambulisha au yanayoweza kutumiwa kumtambulisha binadamu binafsi. Hii inamaanisha kwamba maelezo ya kibinafsi yanajumuisha vitambulishi vya moja kwa moja (kama vile jina) na vitambulishi visivyo vya moja kwa moja (kama vile kitambulisho cha kompyuta au kifaa tamba na anwani ya IP). Tunapotaja wewe au mtumiaji, tunamaanisha mtu anayetumia yoyote ya Huduma hizi. Tunapotaja mdhibiti, tunamaanisha mtu au mhusika ambaye anabainisha ni maelezo gani ya kibinafsi yanayokusanywa kutoka kwako au kukuhusu wewe na jinsi maelezo hayo ya kibinafsi yanatumiwa na kulindwa.

Tunavyokusanya, kutumia na kulinda maelezo yako ya kibinafsi ni chini ya sheria katika maeneo ambako tunaendesha shughuli zetu. Hii inamaanisha kwamba huenda tukawa na mitindo tofauti katika maeneo tofauti.

IKIWA UNA MASWALI KUHUSU JINSI COCA-COLA INAVYOCHAKATA MAELEZO YAKO YA KIBINAFSI, TAFADHALI WASILIANA NA PRIVACY@COCA-COLA.COM.

1. SERA HII INATUMIKA WAKATI GANI?

Sera hii ya Faragha ilichapishwa na inatumika kwa watumiaji wapya kuanzia 16 July 2024.

Matoleo ya hapo mbeleni ya sera za faragha za Coca‑Cola yanatumika mpaka 26 July 2024 na yanapatikana baada ya kutuma ombi kwa privacy@coca-cola.com.

2. SERA HII INATUMIKA WAPI?

Sera ya Faragha inatumika kwa maelezo ya kibinafsi yanayokusanywa kutoka kwa watumiaji wa Huduma kwa ambazo Sera ya Faragha imechapishwa au kuunganishwa, wakati Sera ya Faragha imetajwa katika Huduma au wakati Coca‑Cola inakuomba ukiri unaifahamu. Sera hii ya Faragha pia inasimamia maelezo ya kibinafsi ambayo tunakusanya kutoka kwa watumiaji wanaowasiliana nasi kwa barua pepe, simu na nje ya mtandao, kama vile wakati wa hafla ya kukutana ana kwa ana.

Sera hii ya Faragha pia inatumika kwa maelezo ya kibinafsi tunayopatiwa na watumiaji wanaowasiliana nasi kupitia mitandao ya kijamii. Tafadhali wasiliana nasi kupitia privacy@coca-cola.com ikiwa una maswali kuhusu kama Sera hii ya Faragha inatumika kwa maelezo fulani ya kibinafsi yanayohusiana na mitandao ya kijamii.

Sera hii ya Faragha haitumiki kwa tovuti na huduma nyingine za mtandaoni zinazoendeshwa na mashirika mengine. Tovuti na huduma hizo nyingine zinafuata sera zao binafsi za faragha, si Sera hii ya Faragha. Tafadhali hakikisha kutazama sera hizo za faragha ili ufahamu jinsi maelezo yako yanavyoshughulikiwa.

3. COCA-COLA INAKUSANYA AINA GANI YA MAELEZO NA KWA NINI?

a. Maelezo unayochagua kutupatia

Tunakusanya maelezo ya kibinafsi ambayo unachagua kutusambazia.

Maelezo ya kibinafsi ambayo unachagua kutupatia kwa kawaida yanajumuisha aina zifuatazo za maelezo ya kibinafsi. Tafadhali kagua hapa chini ili kujifahamisha zaidi kuhusu kategoria za maelezo ya kibinafsi ambazo zinakusanywa na Coca‑Cola na kwa nini zinakusanywa:

Maelezo ya Mawasiliano na Akaunti

Coca‑Cola inaomba jina lako la kwanza na la mwisho, anwani ya barua pepe na/au nambari ya simu ya mkononi na tarehe ya kuzaliwa ili kutengeneza akaunti ya Huduma. Pia tunaweza kukusanya jina la mtumiaji na nenosiri, umri, anwani ya kutuma barua, kitambulishi kilichopeanwa na serikali na maelezo sawa ya mawasiliano.

  • Kudumisha akaunti yako ya mtandaoni ukiamua kutengeneza akaunti
  • Kuthibitisha utambulisho na ustahiki kwenye Huduma fulani
  • Kubinafsisha Huduma unazotumia
  • Kukuwezesha kufikia maudhui ya kibinafsi, diskaunti na fursa nyingine
  • Kutayarisha michezo ya bahati nasibu, mashindano na promosheni nyingine au mipango ya kuwashukuru wateja
  • Kukamilisha ununuzi na kuwasilisha bidhaa
  • Kutuma maelezo ambayo tunafikiri kwamba yatakuvutia, ambayo wakati mwingine yanabinafsishwa kulingana na maelezo yanayohusiana na akaunti yako
  • Kuomba maoni yako, kama vile kupitia hojaji kuhusu bidhaa mpya
  • Kujibu maswali yako na kuwahudumia wateja
  • Kwa ajili ya utafiti na uvumbuzi
  • Unapohudhuria hafla ya ana kwa ana, kama vile hafla zilizodhaminiwa au kuandaliwa na Coca‑Cola au kujaribu bidhaa

Maudhui Kutoka kwa Watumiaji (User Generated Content, UGC)

Coca‑Cola inakusanya machapisho, maoni, rekodi za sauti, picha na video ambazo unachagua kuwasilisha kupitia Huduma

  • Kufuatilia jumuiya za mtandaoni
  • Kurekodi na kuchukua hatua kuhusu maoni yako, kama vile katika hojaji, maswali ya huduma kwa wateja na visanduku vingine vya maandishi
  • Kuhudumia ushiriki wako katika promosheni zinazojumuisha uwasilishaji UGC
  • Kuhusiana na ushiriki katika promosheni fulani au Huduma nyingine, kama vile friji maizi za Coca‑Cola.

Picha, rekodi za sauti na video ambazo unachagua kusambaza zinaweza kujumuisha data za bayometriki chini ya baadhi ya sheria. Coca‑Cola inakusanya data za bayometriki pekee kwa idhini yako.

Maelezo yanayohusiana na akaunti iliyo kwenye mfumo wa mtandao wa kijamii

Unapounganisha au kuingia kwenye Huduma kupitia akaunti yako ya mtandao wa kijamii, kama vile Facebook na Twitter, tunakusanya maelezo ya kibinafsi yanayoruhusiwa na mfumo huo wa mtandao wa kijamii na ruhusa za akaunti yako, kama vile picha yako ya wasifu, barua pepe, unachopenda na yanayokuvutia na marafiki, wafuasi au orodha kama hizo.

  • Kubinafsisha Huduma unazotumia
  • Kujibu maoni na maswali yako yaliyochapishwa kwenye mfumo wa mtandao wa kijamii na kuchambua mawasiliano (kama vile tweets au machapisho) ukitumia au kuhusu Coca‑Cola ili kuelewa vyema zaidi jinsi watumiaji wanavyofahamu Coca‑Cola

(Baadaye ukiamua kwamba hautaki kutupatia maelezo kutoka kwenye akaunti yako ya mtandao wa kijamii, basi tafadhali badilisha mipangilio ya faragha kwenye akaunti yako ya mtandao wa kijamii.)

Data za Eneo

Tunakusanya data za eneo haswa la kijiografia (yaani GPS) inaporuhusiwa kupitia Programu zetu unapochagua kuruhusu kupitia mfumo msingi wa uendeshaji wa kifaa chako tamba na vinginevyo kwa idhini yako, inavyohitajika.

Kadirio la eneo kutokana na anwani ya IP au miunganisho kwenye WiFi, Bluetooth au huduma za mtandao pasi waya linakusanywa unapotumia Huduma.

Tunakusanya data hizi za eneo ili:

  • Kubinafsisha Huduma unazotumia
  • Kukufahamisha wakati bidhaa, promosheni au hafla zinapopatikana karibu nawe au kuwawezesha watumiaji wengine kuona eneo lako unapochagua kuruhusu
  • Kutuma matangazo yanayohusiana na eneo la kijiografia

Maelezo mengine ya Kibinafsi yanayosambazwa kupitia Huduma

Tunakusanya ili

  • Kuhudumia jumuiya zetu za mtandaoni
  • Kudhibiti promosheni na vipengele vingine vya Huduma vinavyokuwezesha kusambaza maelezo yako ya kibinafsi

b. Maelezo kuhusu matumizi ya Programu zetu

Unapopakua na kusakinisha mojawapo ya Programu zetu, maelezo tunayokusanya inalingana na mfumo msingi wa uendeshaji na ruhusa za kifaa chako tamba. Programu zetu zinahitaji kutumia vipengele na data fulani kutoka kwenye kifaa chako tamba ili ziweze kufanya kazi. Kwa mfano, ikiwa unataka huduma laini ya mtandaoni hadi kwenye Programu tunahitaji kukusanya na kuunganisha maelezo kutoka kwenye kivinjari chako cha mtandao.

Ili kufahamu zaidi kuhusu maelezo maalum yanayokusanywa na Programu fulani, tafadhali kagua mipangilio ya kifaa chako au kagua maelezo ya ruhusa zinazopatikana kwenye mfumo fulani (k.m. Google Play na App Store) ambapo ulipakua Programu hiyo. Programu fulani pia zinakuwezesha kutazama na kubadilisha hali yako kuhusiana na ukusanyaji wa data fulani katika mipangilio ya Programu. Ukibadilisha mipangilio yako, vipengele fulani vya Programu huenda kikakosa kufanya kazi ipasavyo.

Ili kusitisha ukusanyaji wa maelezo yote kupitia Programu fulani, tafadhali futa Programu hiyo.

c. Maelezo yanayokusanywa kiotomatiki wakati wa kutumia Huduma

Tunakusanya maelezo fulani kiotomatiki kuhusu na kutokana na matumizi ya Huduma kutoka kwenye kompyuta na vifaa tamba vya watumiaji. Baadhi ya maelezo yanayokusanywa kiotomatiki ni maelezo ya kibinafsi chini ya sheria fulani. Maelezo haya yanakusanywa kiotomatiki kwa kutumia kuki, pixel, web beacons na teknolojia kama hizo za kukusanya data (kwa pamoja, teknolojia ya ukusanyaji data).

Maelezo yanayokusanywa kiotomatiki yanajumuisha:

  • maelezo kuhusu kompyuta yako au kifaa chako tamba, kama vile aina ya kifaa na nambari ya utambulisho, aina ya kivinjari, mtoa huduma ya intaneti, mtandao wa simu na mfumo msingi wa uendeshaji
  • anwani ya IP na eneo pana la kijiografia (k.m. nchi au eneo la mji)
  • jinsi kompyuta au kifaa tamba kinavyotangamana na Huduma, pamoja na tarehe na saa ambapo Huduma zilitumika, maombi na matokeo ya utafutaji, ubonyezaji na mwenendo wa kipanya, kurasa halisi za tovuti zilizofunguliwa, viungo viulivyobonyezwa na video zilizotazamwa
  • vipimo vya trafiki na matumizi
  • data kuhusu tovuti na huduma za wahusika wengine zilizotumiwa kabla ya kutangamana na Huduma, ambazo zinatumika kufanya matangazo kuwafaa watumiaji zaidi
  • mitagusano na mawasiliano yetu ya uuzaji, kama vile kama na ni wakati gani barua pepe ya Coca‑Cola ilifunguliwa

d. Maelezo yanayokusanywa kutoka kwa wahusika wengine

Mara kwa mara, tunapokea maelezo ya kibinafsi kutoka kwa wahusika wengine ambayo tunatumia kufahamu zaidi kuhusu watumiaji wetu, kubinafsisha huduma za watumiaji na kwa ufanisi zaidi kutangaza na kuboresha Huduma.

Aina za maelezo ya kibinafsi tunazopokea kutoka kwa wahusika wengine ni:

  • Maelezo ya kibinafsi yanayohusishwa na ununuzi. Ununuzi wa kadi ya malipo unachakatwa na mifumo ya kuchakata malipo ya wahusika wengine. Coca‑Cola haina nambari kamili za akaunti za benki, nambari za kadi za mkopo au nambari za kadi za salio.
  • Maelezo ya kibinafsi ambayo yanapatikana kibiashara kutoka kwa watoa huduma za uuzaji au yaliyokusanywa na washirika wa uuzaji kupitia kampeni na hafla, ambayo yanatumika kusaidia kuwatambua watu binafsi ambao huenda wangependa kujifunza zaidi kuhusu Coca‑Cola na kuchangia kwenye maelezo ya kibinafsi ambayo tayari tunayo. Maelezo haya ya kibinafsiyanajumuisha michango kutokana na kulinganisha data zetu tulizoondolea majina dhidi ya data za wahusika wengine zilizoondolewa majina, pamoja na vyumba vya kukusanya data (pia tazama Sehemu ya 4 hapa chini).
  • Maelezo ya kibinafsi tunayokusanya kutoka kwa washirika wengine wa matangazo wanaotusaidia kutoa matangazo yanayofaa zaidi
  • Maelezo ya kibinafsi yanayosambawa kwa Coca‑Cola na washirika wa kuweka bidhaa kwenye chupa
  • Maelezo ya kibinafsi kutoka kwenye vyanzo vinavyopatikana hadharani
  • Maelezo ya kibinafsi kutoka kwa mashirika ya utekelezaji sheria na mamlaka nyingine za serikali (lakini katika matukio nadra pekee)

Tunaweza kuunganisha maelezo ambayo Coca‑Cola iko nayo kukuhusu au kuunganisha data kutoka kwa vyanzo vingine vya data. Tunamhitaji kila mtoa huduma mwingine kuthibitisha kwamba yeye kusambazia Coca‑Cola maelezo ya kibinafsi ni wazi kwa watumiaji na ni halali.

e. Maelezo mengine yanayokusanywa kwa idhini yako

Tunaweza kukuomba idhini yako ili kukusanya aina maalum za maelezo ya kibinafsi ili uweze kushiriki katika shughuli mpya, kupokea maelezo ya kipekee au kujaribu vipengele vipya. Chini ya baadhi ya sheria za faragha, Coca‑Cola inahitajika kupata idhini kabla ya kukusanya na kutumia maelezo ya kibinafsi. Tafadhali tazama Sehemu ya 9 ili kupata maelezo ya kina.

4. COCA-COLA INATUMIA MAELEZO YA KIBINAFSI VIPI?

Coca‑Cola inatumia maelezo ya kibinafsi ili kutoa na kuboresha Huduma, kudhibiti biashara yetu, kulinda watumiaji na kutekeleza haki zetu za kisheria.

Tunatumia maelezo ya kibinafsi ili kutoa, kubinafsisha na kuboresha Huduma (katika kila tukio kama inavyoruhusiwa na sheria husika), pamoja na:

  • Kutengeneza na kusasisha akaunti za watumiaji na kutimiza maombi ya watumiaji
  • Kuhifadhi pamoja maelezo ya kibinafsi ya watumiaji kwenye hifadhidata inayodhibitiwa na mhusika mwingine kwa niaba yetu na kuambatisha maelezo yaliyokusanywa kutoka kwa wahusika wengine
  • Kutuma mawasiliano ya uuzaji na yasiyo ya uuzaji kwa watumiaji
  • Kuwezesha mawasiliano miongoni mwa watumiaji, kama vile jumuiya ya mtandaoni
  • Kwa matangazo lengwa (pia wakati mwingine yanaitwa natangazo yaliyobinafsishwa au kulingana na mvutio) kulingana na maelezo yaliyotokana na shughuli za mtandaoni za mtumiaji, kama vile kutembelea tovuti zilizo na matangazo au kuki za washirika wetu wa matangazo, ambayo baadhi yake yanalingana na eneo la kijografia.
  • Kujifahamisha zaidi kuhusu watumiaji wetu ili tuweze kupendekeza maudhui ambayo tunafikiria yatawavutia watumiaji fulani
    • Haswa, tunapata maelezo kuhusu watumiaji kwa kushiriki katika ‘vyumba vya kukusanya data.’ Kupitia chumba cha kukusanya data, tunaendesha maswali na kupata matokeo kutokana na data zinazotolewa na wahusika wengine ambao pia wanashiriki. Data zinazotumika kwenye vyumba vya kukusanya data zinasambazwa na biashara zingine na washiriki wengine kwa mfumo ambao haufichui moja kwa moja maelezo ya kibinafsi; badala yake, kabla ya kulinganisha, kitambulishi kinatengenezwa na kutumiwa kulinganisha data za wahusika wengine dhidi ya maelezo ya kibinafsi yaliyoondolewa jina ya Coca‑Cola. (Kutumia maelezo ya kibinafsi kwa malengo ya kutengeneza data zilizoondolewa jina kunahusisha uainishaji awali wa data.)  Baada ya mchakato wa kulinganisha, tunapokea maelezo yaliyokadiriwa kuhusu hadhira yetu ambao hawaruhusu uimarishaji wa data binafsi isipokuwa tukufahamishe au kupata idhini tofauti. Usambazaji wa data katika vyumba vya kukusanya data ni kwa malengo ya ugunduaji hadhira, upanuaji hadhira, ulengaji hadhira na uigaji hadhira zinazofanana.
  • Ili kudhibiti mipango ya promosheni na kuwazawadi wateja
  • Ili kutoa huduma kwa wateja
  • Ili kuwezesha malipo
  • Kuchambua jinsi watumiaji wanavyotangamana na Huduma na mitindo ya shughuli ili tuweze kutengeneza vipengele na maudhui mapya ambayo yanatimiza matarajio ya watumiaji wetu
  • Kuboresha Huduma na hisia za watumiaji kuzihusu
  • Ili kufanya uchambuzi wa data, utafiti, utengenezaji bidhaa na machine learning ambazo zinatuwezesha kuelewa watumiaji wetu vyema zaidi na kutoa kufanya uvumbuzi kwa ajili yao
  • Ili kufuatilia na kujaribu Huduma, pamoja na kusuluhisha matatizo ya operesheni
  • Kutengeneza data zilizoondolewa data, ambazo haziko chini ya Sera hii ya Faragha, ambazo zinatumika katika kuboresha bidhaa na huduma za Coca‑Cola na malengo sawa ya biashara na vinginevyo kama inavyoruhusiwa na mkataba na sheria
  • Kugundua na kulinda dhidi ya ulaghai, matumizi mabaya na bila idhini ya Huduma
  • Kwa malengo ya kudhibiti hatari na ya kimamlaka, kama vile kufuatilia na kutekeleza uambatanaji na makubaliano ya watumiaji na vinginevyo kuambatana na sheria zinazotumika na Coca‑Cola

5. COCA-COLA INATUMIA KUKI NA TEKNOLOJIA NYINGINE ZA KUKUSANYA DATA?

Tunatumia kuko na teknolojia nyingine za kukusanya data ili kukutambua wewe na/au vifaa vyako unapotumia Huduma na kukusanya maelezo ya kibinafsi kukuhusu.

Katika baadhi ya matukio nadra, kunaweza kuwa na baadhi ya tovuti ambazo ni sehemu ya Huduma ambazo zina ilani maalum kuhusu kuki na teknolojia nyingine za kukusanya data zinazotumika kwenye tovuti na watumiaji maalum. Ukitembelea tovuti ya Coca‑Cola iliyo na ilani kuhusu kuki, basi ilani ya kuki ya tovuti hiyo inatumika.

Kuki ni nini?
Kuki ni faili ndogo za maandishi ambazo zinatumwa au kufikiwa kwenye kivinjari chako cha mtandao au hifadhi ya kompyuta yako. Kwa kawaida kuki ina jina la tovuti (eneo la intaneti) ambapo kuki ilitoka, “muda wa kudumu” wa kuki (yaani itakapoishiwa na muda) na nambari ya kipekee iliyotengenezwa bila mpangilio maalum au kitambulishi kama hicho,. Pia kuki inaweza kuwa na maelezo kuhusu kompyuta au kifaa chako, kama vile mipangilio, historia ya kuvinjari na shughuli zinazofanywa unapotumia Huduma.

Pia Coca‑Cola inatumia “pixels” (wakati mwingine web beacons). Pixels ni picha wazi zinazoweza kukusanya maelezo kuhusu kufunguliwa kwa barua pepe na matumizi ya tovuti mbali mbali na kwa muda fulani.

Kuki zinazotumiwa na Coca‑Cola kwenye Huduma zinaitwa kuki za mhusika halisi. Kuki zinazotumiwa na mhusika mwingine yeyote zinaitwa kuki za mhusika mwingine. Kuni za mhusika mwingine zinawezesha vipengele ua utendaji wa mhusika mwingine kwenye au kupitia Huduma, kama vile takwimu na ufanyaji uuzaji kuwa otomatiki. Wahusika wanaotumia kuni za mhusika mwingine zinaweza kutambua kifaa chako unapokitumia kufikia Huduma na pia wakati unapokitumia kufikia tovuti nyingine. Ili kujifunza mengi zaidi kuhusu kuki kwa ujumla, tembelea www.allaboutcookies.org.

Baadhi ya vivinjari vya mtandao (pamoja na Safari, Internet Explorer, Firefox na Chrome) zinajumuisha “Do Not Track” (DNT) au kipengele sawia kinachoeleza tovuti kwamba mtumiaji hataki shughuli au tabia zake za mtandaoni kufuatiliwa. Tovuti inayojibu ishara fulani ya DNT inapopokea ishara ya DNT, kivinjari kinazuia tovuti hiyo kukusanya maelezo fulani kutoka kwenye kashe ya kivinjari. Si vivinjari vyote vina chaguo la DNT na ishara za DNT bado hazina mpangilio sawa. Kwa sababu hii, watoa huduma za tovuti wengi, pamoja na Coca‑Cola, bado hawajibu ishara za DNT.

Kwa nini Coca‑Cola inatumia kuki na teknolojia nyingine za kukusanya data?

Baadhi ya kuki zinahitajika ili Huduma kufanya kazi. Kuki zingine zinatuwezesha kufuatilia mambo yanayowavutia watumiaji kwa ajili ya matangazo lengwa na ili kuimarisha Huduma.

Aina za kuki zinazotumiwa kupitia Huduma na kwa nini zinatumiwa ni kama ifuatavyo:

  • Kuki muhimu kabisa zinahitajika ili Huduma kufanya kazi.
  • Kuki za Utendaji au Uchambuzi zinakusanya maelezo kuhusu jinsi Huduma zinatumiwa ili tuweze kuchambua na kuboresha Huduma. Kuki za utendaji na uchambuzi kwa kawaida zinasalia kwenye kompyuta yako baada ya kufunga kivinjari chako mpaka wakati unakapozifuta.
  • Kuki za Matangazo zinatumika kufanya jumbe za matangazo kukufaa zaidi kwa kutusaidia kuonyesha matangazo ambayo yanalingana na mambo uliyoashiria kuwa yanakuvutia, kuzuia tangazo sawa kujirudia rudia mara nyingi na kuhakikisha matangazo yanaonyeshwa inavyofaa kwa niaba ya watangazaji.
  • Kuki za mitandao ya kijamii zinawawezesha watumiaji kutangamana kwa urahisi zaidi na mifumo ya mitandao ya kijamii. Hatudhibiti kuki za mitandao ya kijamii na hazituruhusu kufikia akaunti zako za mitandao ya kijamii bila idhini yako. Tafadhali rejelea sera husika ya faragha ya mfumo wa mtandao wa kijamii ili kupata maelezo kuhusu kuki zinazotumiwa.

Teknolojia ya kukusanya data inawezesha Coca‑Cola kufuatilia mtindo wa trafiki kutoka ukurasa mmoja wa tovuti hadi ule mwingine, ili kuwasilisha au kuwasiliana na kuki, ili kuelewa kama watumiaji wanatembelea Huduma baada ya kuona tangazo letu la mtandaoni lililoonyeshwa kwenye tovuti ya mhusika mwingine, ili kuboresha utendaji wa Huduma na kukadiria mafanikio ya kampeni zetu za uuzaji wa barua pepe. Sera za Kuki za Coca‑Cola (zinapatikana katika mamlaka fulani) zinaelezea matumizi ya teknolojia ya kukusanya data na Coca‑Cola. 

Bidhaa za Google

Inaporuhusiwa na sheria husika, Huduma zinatumia Takwimu za Google kwa matangazo lengwa (ambayo wakati mwingine Google inayarejelea kama ‘remarketing’). Google inatumia kuki ambazo Google inatambua wakati watumiaji wanapotembelea tovuti mbalimbali. Data zinazokusanywa kupitia kuki za Google zinasaidia Coca‑Cola kuchambua jinsi Huduma zinavyotumiwa na, kwa baadhi ya Huduma na katika baadhi ya mamlaka, kubinafsisha mawasiliano ya uuzaji na matangazo ya kidijitali.

Pia Huduma zinaambatisha video kutoka kwa YouTube (kampuni moja ya Google) kwa kuweka kwenye fremu. Hii inamaanisha kwamba, baada ya kubonyeza kitufe cha kucheza video ya YouTube kupitia Huduma, muunganisho kati ya Huduma na seva za YouTube unaanzishwa. Kisha, kiungo cha HTML kinachotolewa na YouTube kinawekwa kwenye programu ya Huduma ili kutengeneza fremu ya uchezaji. Kisha video iliyohifadhiwa kwenye seva za YouTube inachezwa na fremu hiyo ndani ya Huduma. Pia YouTube inapokea maelezo yanayoifahamisha YouTube kwamba kwa sasa unatumia Huduma: anwani yako ya IP, maelezo ya kivinjari, mfumo msingi wa uendeshaji na mipangilio ya kifaa unachotumia, URL ya ukurasa wa sasa wa tovuti, kurasa za tovuti ulizotembelea hapo awali ikiwa umefuata kiungo fulani, na video ulizotazama. Ikiwa uliingia kwenye akaunti yako ya YouTube, maelezo haya huenda yakahusishwa na wasifu wako wa mtumiaji wa YouTube. Unaweza kuzuia uhusiano huu kwa kutoka nje ya akaunti yako ya YouTube kabla ya kutumia Huduma na kufuta kuki husika. 

Ili kupata maelezo zaidi kuhusu jinsi Google inavyokusanya, kutumia na kusambaza maelezo yako, tafadhali tembelea Sera ya Faragha ya Google

Ili kupata maelezo zaidi kuhusu jinsi Google inavyotumia kuki katika matangazo, tafadhali tembelea ukurasa wa Matangazo wa Google.

Ili kuzuia Google Analytics kutumia data zako, unaweza kusakinisha programu jalizi ya kujiondoa ya kivinjari ya Google.

Ili kujiondoa kwenye matangazo ya Google ambayo yanalengwa kulingana na mambo yanayokuvutia, tumia mipangilio yako ya matangazo ya Google

Ikiwa unaishi katika EEA, Uswizi au Uingereza, tafadhali kumbuka haswa kwamba, ukiruhusu kuki za Google kwenye Kituo cha Mapendeleo ya Faragha cha Coca‑Cola, maelezo yanayotokana na kuki hizi kuhusu matumizi ya Huduma yanawasilishwa na kuhifadhiwa na seva za Google nchini Marekani. Coca‑Cola ilitumia zana za teknolojia, pamoja na zana ya Google ya Kuondoa Utambulisho wa IP, ili kuondoa sehemu ya mwisho ya anwani ya IP kabla ya data kutumwa na Google hadi Marekani, na pia zana za Google za kulemaza usambazaji data na mipangilio ya Google ya ishara na Kitambulisho cha Mtumiaji katika Google Analytics kwenye maeneo fulani ya mamlaka. Google haitahusisha anwani ya IP na data nyingine zozote zinazohifadhiwa na Google.

Kwa niaba ya Coca‑Cola, Google itatumia data zilizobainishwa hapa juu ili kutayarisha ripoti zinazosaidia Coca‑Cola kuendesha na kutoa Huduma.

Bidhaa za Meta

Baadhi ya sehemu ya Huduma inatumia bidhaa na vipengele vinavyotolewa na Facebook, Instagram na Messenger na programu za Facebook (Bidhaa za Meta). Bidhaa za Meta zinatumia tagi, pixels (Meta Pixel) na programu na teknolojia zingine za kipekee za kufuatilia zinazokusanya maelezo ya mtumiaji (pamoja na maelezo ya kibinafsi) kutoka kwa Huduma. Facebook inafuatilia mitagusano na Huduma baada ya mtumiaji kubonyeza tangazo lililowekwa kwenye Facebook au huduma nyingine zinazotolewa na Meta (inaitwa mafanikio) na inawezesha Coca‑Cola kujua mengi zaidi kuhusu jinsi watumiaji wanavyotangamana na matangazo na maelezo sawa.  Bidhaa za Meta zinatumia data zilizokusanywa kwa malengo ya Meta, pamoja na kuboresha Bidhaa za Meta. Meta inaweza kuhamisha data ambazo inakusanya kutoka kwa Huduma hadi nchini Marekani na nchi nyingine, ambapo unaweza kuwa na haki chache zaidi zinazohusiana na maelezo yako ya kibinafsi. Ili kujifunza kuhusu jinsi Bidhaa za Meta zinavyokusanya, kutumia na kuchakata maelezo ya kibinafsi na jinsi unavyoweza kudhibiti au kufuta maelezo ya kibinafsi kukuhusu wewe, tafadhali tazama Sera ya Faragha ya Bidhaa za Meta kwenye https://www.facebook.com/about/privacy.

Machaguo Yako ya Kuki

Unaweza kupanga kivinjari chako kikatae kuki zote au kuonyesha wakati kuki inapowekwa. (Vivinjari vingi vinakubali kuki kiotomatiki lakini vinakuruhusu kuzilemaza lakini kumbuka kwamba baadhi ya vipengele vya huduma vinaweza kukosa kufanya kazi vizuri bila kuki.)

Kama ilivyotajwa hapa juu, Google imetengeneza programu jalizi ya kujiondoa ya kivinjari ikiwa unataka kujiondoa kwenye kuki zinazotumika na Google Analytics. Unaweza kupakua na kusakinisha programu jalizi ya kivinjari chako hapa. Unaweza kukataa matumizi ya kuki hizi kwa kuchagua mipangilio mwafaka kwenye kivinjari chako. Ili kujifunza mengi zaidi kuhusu jinsi ua kutazama na kudhibiti maelezo yako kwenye Bidhaa za Meta, tafadhali tazama hapa.

Maeneo fulani ya mamlaka ambako Huduma zinapatikana pia yana sera za kuki ambazo ni tofauti na zinajumuishwa kwenye Sera hii ya Faragha na zana za kudhibiti kuki. Tafadhali rejelea Sehemu ya 9 ili kupata maelezo ya kina. 

6. COCA-COLA INASAMBAZA MAELEZO YA KIBINAFSI VIPI?
Coca‑Cola inasambaza maelezo ya kibinafsi kwa watu na biashara zinazosaidia kuendesha Huduma na kufanya biashara yetu na wakati tunaruhusiwa au tunahitajika kisheria kusambaza. Pia tunasambaza maelezo ya kibinafsi wakati mtumiaji anapoomba tuyasambaze. Tunahitaji wapokeaji wa maelezo ya kibinafsi kutoka kwetu waambatane na Sera hii ya Faragha isipokuwa na mpaka wakati watumiaji wanafahamishwa kwamba sera au ilani tofauti ya faragha itatumiwa.

Coca‑Cola inasambaza maelezo ya faragha kwa kategoria zifuatazo za wapokeaji:

  • Washauri wataalam, kama vile mawakili, wahasibu, watoa bima na wataalamu wa uchunguzi na usalama wa maelezo.
  • Wachuuzi wa uuzaji wanaosaidia kutangaza Huduma (kama vile uuzaji wa barua pepe) na mara kwa mara kutumia maelezo ya kibinafsi ambayo tayari tuko nayo. Kwa mfano, Meta inapokea na kutumia data fulani zinazohusiana na matumizi ya Huduma ili kutusaidia kuwasilisha matangazo yaliyobinafsishwa kwenye mfumo wao na kitathmini ufanisi wa utangazaji huu.
  • Watoa huduma kuwawezesha kutekeleza huduma kwa niaba yetu, ikijumuisha uchambuzi wa data, usalama wa data, shughuli za biashara mtandaoni, utafiti, utekelezaji promosheni, ofa na mipango ya kuwazawadi wateja na vinginevyo kutusaidia kuendesha biashara yetu. Baadhi ya watoa huduma hawa wana majukumu kote ulimwenguni.
  • Kwa ushirika wa kimkakati, kama vile na ligi za spoti na watengenezaji na watoa huduma wengine wa ofa za zawadi.
  • Kupitia vyumba vya kukusanya data kama ilivyobainishwa katika Sehemu ya 4. Usambazaji wa data katika chumba cha kukusanya data ni kwa malengo ya kugundua hadhira, kupanua hadhira, kulenga hadhira na kuiga hadhira zinazofanana.
  • Watoa huduma za kuhifadhi data.
  • Wanunuzi au wawekezaji wa siku zijazo au halisi na washauri wao wa kitaalamu kuhusiana na muunganiko, ununuzi au uwekezaji wowote halisi au uliopendekezwa katika au wa sehemu zote au yoyote ya biashara yetu. Tutafanya juhudi zetu bora ili kuhakikisha kwamba masharti yote ya Sera hii ya Faragha yanatumika kwa maelezo ya kibinafsi baada ya muamala au kwamba watumiaji wanapokea ilani za awali kuhusu mabadiliko kwenye uchakataji wa maelezo ya kibinafsi.
  • Washirika wa Coca‑Cola na wabia wa kuweka bidhaa kwenye chupa.
  • Watekelezaji sheria, wadhibiti wa serikali na mahakama adilifu wakati tunaamini ufichuaji ni muhimu (i) ili kuambatana na sheria, (ii) ili kutekeleza, kuweka na kulinda haki za kisheria, au (iii) ili kulinda nia muhimu za watumiaji, wabia wa kibiashara, watoa huduma au mhusika mwingine.
  • Wahusika wengine kwa idhini yako.

Tunaposambaza maelezo ya kibinafsi, tunahitaji kwamba wapokeaji washughulikie maelezo ya kibinafsi kwa kuambatana na Sera hii ya Faragha na mahitaji yetu ya usiri na usalama. 

7. COCA-COLA INALINDA MAELEZO YA KIBINAFSI VIPI?
Coca‑Cola inachukua tahadhari ili kulinda maelezo ya kibinafsi ambayo tumeaminiwa kuhifadhi. Tunatumia hatua mbalimbali ili kutusaidia kulinda maelezo ya kibinafsi dhidi ya ufikiaji na matumizi bila idhini.

Coca‑Cola inatumia vizuizi vya kiufundi, halisia, na kiutawala vinavyokusudiwa kulinda maelezo ya kibinafsi ambayo tunachakata. Vizuizi vyetu vimebuniwa kuwa ngazi ya usalama inayofaa hatari ya uchakataji maelezo yako ya kibinafsi na kujumuisha (inapofaa) hatua za kuhakikisha usiri, uadilifu, upatikanaji, na uthabiti endelevu wa mifumo ya kuchakata na utaratibu wa kufanya majaribio, kutathmini, na kukagua mara kwa mara ufanisi wa hatua za kiufundi na kimpangilio za kuhakikisha usalama wa kuchakata maelezo ya kibinafsi. Hata hivyo, Coca‑Cola haiwezi kuondoa kikamilifu hatari za kiusalama zinazohusishwa na uchakataji wa maelezo ya kibinafsi.

Una wajibu wa kudumisha usalama wa maelezo ya kuingia kwenye akaunti yako. Coca‑Cola itachukulia kwamba ufikiaji wa Huduma kupitia maelezo yako ya kuingia kwenye akaunti yako kuwa umeidhinishwa nawe.

Coca‑Cola inaweza kusitisha matumizi yako ya Huduma yote au sehemu yake bila ilani tukituhumu au kugundua ukiukaji wowote wa usalama. Ikiwa unaamini kwamba maelezo uliyopatia Coca‑Cola au akaunti yako si salama tena, tafadhali tuarifu mara moja kupitia Privacy@coca-cola.com.

Tukipata habari kuhusu ukiukaji unaoathiri usalama wa maelezo yako ya kibinafsi, tutakupa ilani inavyohitajika na sheria husika. Inaporuhusiwa na sheria husika, Coca‑Cola inakupa ilani hii kwa kutumia anwani ya barua pepe inayohusishwa na akaunti yako au mbinu nyingine iliyoidhinishwa inayohusishwa na akaunti yako.

UFIKIAJI BILA IDHINI WA MAELEZO YA KIBINAFSI KUPITIA HUDUMA – PAMOJA NA UPEKUZI – UMEPIGWA MARUFUKU NA INAWEZA KUPELEKEA MASHATAKA YA KIJINAI.

8. COCA-COLA INAHIFADHI MAELEZO YA KIBINAFSI KWA MUDA GANI?
Tunahifadhi maelezo ya kibinafsi kuhusu mtumiaji mradi akaunti ya mtumiaji ni amilifu na vinginevyo mradi iwe ni muhimu kwa malengo yaliyobainishwa hapa juu. Pia tunahifadhi maelezo ya kibinafsi mradi iwe ni muhimu ili kuambatana na majukumu ya kisheria, kusuluhisha migogoro, na kutekeleza mikataba yetu.

Tunakusudia kudumisha maelezo yako ya kibinafsi ikiwa sahihi na imesasishwa. Tunahifadhi maelezo ya kibinafsi tunayoshughulikia chini ya Sera hii ya Faragha kulingana na sera yetu ya kuhifadhi data.  Wakati wa kubainisha kipindi cha kuhifadhi, tunazingatia vigezo mbalimbali, kama vile aina ya bidhaa na huduma unazoomba au unazopatiwa, hali na urefu wa uhusiano wetu nawe na vipindi vya lazima vya kuhifadhi chini ya sheria husika. Mwishoni mwa kipindi husika cha kuhifadhi, tunafuta au kuondoa utambulisho kwenye maelezo ya kibinafsi au, ikiwa hatuwezi kufuta au kuondoa utambulisho kwenye maelezo ya kibinafsi, kisha tunatenganisha na kuhifadhi maelezo ya kibinafsi kwa njia salama mpaka wakati wa kufuta au kuondoa utambulisho utakapowezekana.

Baada ya kuondoa utambulisho kwenye maelezo ya kibinafsi, si maelezo ya kibinafsi tena. Tunatumia data bila utambulisho chini ya sheria na mikataba husika.

9. KUNA MACHAGUO GANI KUHUSIANA NA MAELEZO YA KIBINAFSI?

Unaweza kufanya machaguo kuhusu Coca‑Cola kushughulikia maelezo yako ya kibinafsi. Unaweza kutumia haki zako za faragha kwa kuwasiliana na Coca‑Cola kama ilivyobainishwa katika Sehemu hii ya 9 au kutumia zana mbalimbali zinazopatikana kupitia kivinjari chako au ambazo zinatolewa na Coca‑Cola. Katika baadhi ya matukio, uwezo wako wa kufikia au kudhibiti maelezo yako ya kibinafsi unapunguzwa na sheria husika.

Mapendeleo ya Kifaa Tamba
Mifumo msingi ya uendeshaji vifaa tamba na mifumo ya programu (k.m. Google Play, App Store) ina mipangilio ya ruhusa kwa aina maalum ya data na arifa za vifaa tamba, kama vile ruhusa za kufikia wasiliani, huduma za maeneo ya kijiografia na arifa za papo hapo. Unaweza kutumia mipangilio iliyo kwenye kifaa chako tamba ili kuidhinisha au kukataza ukusanyaji wa maelezo fulani na/au arifa za papo hapo. Pia Programu fulani zinaweza kuwa na mipangilio inayokuwezesha kubadilisha ruhusa na arifa za papo hapo. Kwa baadhi ya Programu, kubadilisha mipangilio kunaweza kufanya vipengele fulani vya Programu kutofanya kazi ipasavyo.

Unaweza kusitisha ukusanyaji wote wa maelezo kutoka kwa Programu kwa kufuta Programu hiyo. Ukifuta Programu, tafadhali zingatia kukagua mipangilio yako ya mfumo msingi wa uendeshaji ili kuthibitisha kwamba kitambulishi cha kipekee na shughuli nyingine zinazohusishwa na matumizi yako ya Programu kimefutwa kwenye kifaa chako tamba. 

Kujiondoa kwenye Barua Pepe na Arafa za Coca‑Cola
Ili kuacha kupokea barua pepe za matangazo kutoka kwa Coca‑Cola, tafadhali bonyeza kiungo cha “Jiondoe” kilicho katika sehemu ya chini ya barua pepe hiyo. Baada ya kujiondoa, bado tunaweza kukutumia mawasiliano yasiyo ya matangazo, kama vile risiti za ununuzi au maelezo ya kiutawala kuhusu akaunti yako.

Pia mipangilio ya akaunti yako inakuwezesha kubadilisha mapendeleo yako ya arifa, kama vile arifa za papo hapo kutoka kwa Programu.

Ili kuacha kupokea arafa za matangazo (SMS au MMS), tafadhali tuma arafa ya jibu inayoonyesha kwamba ungependa kuacha kupokea arafa za matangazo kutoka kwetu – kama vile kutuma arafa ya neno “Stop”. Pia unaweza kutufahamisha kama ilivyoelekezwa hapa chini kwenye sehemu ya “Wasiliana Nasi”. Tafadhali bainisha ni aina gani za mawasiliano ambazo hautaki tena kupokea pamoja na nambari husika ya simu, anwani, na/au anwani ya barua pepe. Ukijiondoa kupokea jumbe zinazohusiana na uuzaji kutoka kwetu, bado tunaweza kukutumia jumbe muhimu za kiutawala, kama vile barua pepe kuhusu akaunti zako au ununuzi wako

MAELEZO KUHUSU HAKI NA MACHAGUO YA FARAGHA YA MAENEO FULANI YA MAMLAKA YAMETOLEWA KATIKA SEHEMU YA 13 MWISHONI MWA SERA HII YA FARAGHA. TUNAKUHAMASISHA UPITIE SEHEMU HUSIKA.

IKIWA UNAISHI KATIKA ENEO LA MAMLAKA LILILO NA SHERIA ZA FARAGHA ZINAZOKUPA HAKI ZA FARAGHA AMBAZO HAZIJABAINISHWA KATIKA SERA HII YA FARAGHA, TAFADHALI WASILIANA NASI KUPITIA PRIVACY@COCA-COLA.COM. Tunaheshimu haki zako za faragha na tutafanya juhudi zetu bora ili kutimiza maombi yako.

10. COCA-COLA INALINDA FARAGHA YA WATOTO VIPI?
Baadhi ya Huduma zima masharti ya umri kumaanisha kwamba tunaweza kuuliza maswali ili kuthibitisha umri wako kabla tukuruhusu kutumia Huduma hizo.

Kulingana na Sera yetu ya Uuzaji kwa Kuwajibika, Coca‑Cola haielekezi uuzaji wa bidhaa zetu kwa watoto walio na umri wa chini ya miaka 13. Ukijua kwamba mtoto aliye na umri wa chini ya miaka 13 au umri uliowekwa chini ya sheria za eneo lako ametupatia maelezo ya kibinafsi bila idhini ya mzazi au bila ruhusa ya sheria husika, tafadhali wasiliana na Ofisi yetu ya Faragha kupitia privacy@coca-cola.com. Tukipata habari kuhusu tutachukua hatua kuondoa maelezo ya kibinafsi ya mtoto huyo inavyohitajika na sheria husika.

11. COCA-COLA INAHAMISHA MAELEZO YA KIBINAFSI HADI NCHI ZINGINE?

Coca‑Cola inaweza kutuma maelezo ya kibinafsi nje ye mipaka hadi maeneo yoyote ambako sisi na waletaji wetu na washirika wetu wa biashara tunaendesha shughuli. Maeneo haya mengine yanaweza kuwa a sheria za ulindaji data ambazo ni tofauti (na, wakati mwingine, hazina ulinzi tosha) na sheria za mahali unakoishi.

Tukituma maelezo yako ya kibinafsi nje ya mipaka au kwa niaba yetu, tunatumia vizuizi mwafaka ili kulinda maelezo yako ya kibinafsi kulingana na Sera hii ya Faragha na sheria husika. Vizuizi hivi vinajumuisha kukubali mikataba ya kawaida au mikataba ya kuigwa ya kutuma maelezo ya kibinafsi miongoni mwa washirika wa Coca‑Cola na miongoni kwa waletaji na wabia wetu. Inapotumika, mikataba hii inawahitaji washirika, waletaji na wabia kulinda maelezo ya kibinafsi kulingana na sheria husika za faragha.

Ili kuomba maelezo kuhusu mikataba yetu ya kawaida au vizuizi vingine vya utumaji maelezo ya kibinafsi nje ya mipaka, tafadhali wasiliana na privacy@coca-cola.com.

12. SERA HII YA FARAGHA INABADILISHWA LINI?
Mara kwa mara tunaweza kusasisha Sera hii ya Faragha kulingana na mabadiliko ya kisheria, kiufundi na kibiashara. Toleo mpya zaidi litapatikana kupitia Huduma.

Tunaposasisha Sera hii ya Faragha, tutachapisha toleo jipya zaidi na kubadilisha Tarehe ya Kuanza Kutumika hapa juu. Pia tunachukua hatua mwafaka kukufahamisha mapema kuhusu mabadiliko makubwa ambayo tunaamini yanaathiri haki zako za faragha ili uwe na fursa ya kukagua Sera ya Faragha iliyorekebishwa kabla ianze kutumika. Ikiwa idhini yako inahitajika na sheria husika za faragha, tunapata idhini yako kuhusu mabadiliko kabla ya Sera ya Faragha iliyorekebishwa ianze kutumika kwako. Tafadhali kagua Sera hii ya Faragha mara kwa mara ili kuhakikisha unafahamu toleo jipya zaidi.