Imagine Dragons
Imagine Dragons wameendelea kutufundisha namna muziki wa Rock unafanywa kwenye karne ya 21. Kuanzia Kujaza viwanja vya michezo, kutengeneza nyimbo zinazopendwa na wengi, na kuvunja rekodi kila kukicha, washindi hao wa tuzo za GRAMMY® kutoka Las Vegas, Imagine Dragons wamechukua nafasi yakipekee kama mojawapo ya bendi kubwa zaidi za Rock duniani. Kwa kujumlisha mauzo ya albamu sawa na milioni 66, nyimbo za kidijitali milioni 55, na strimu bilioni 110, na wanasimama kama “bendi pekee katika historia nyimbo zao nne kupata heshima ya dhababu kutoka RIAA, nyimbo hizo ni " “Radioactive” (14x-platinum), “Believer” (10x-platinum), “Demons” (10x-platinum), and “Thunder” (10x-platinum). Tangu walipoibuka mwaka 2009, wameingia mara tano mfululizo kwenye top 10 ya nyimbo zilizotoka kwenye chat za Billboard Top 200 kupitia nyimbo kama Night Visions [2012] (7x-platinum) (KIDinaKORNER/Interscope), Smoke + Mirrors [2015] (platinum) (KIDinaKORNER/Interscope), Evolve [2017] (triple-platinum) (KIDinaKORNER/Interscope), Origins [2018] (platinum)( KIDinaKORNER/Interscope), na Mercury – Act 1 [2021]( KIDinaKORNER/Interscope). Pamoja kutoa wimbo wa Mercury - Act 2(KIDinaKORNER/Interscope), mwaka 2022 walikamilisha kutoka Albam mbili kwa Pamoja Opus chini ya nguli Rick Rubin. Wimbo maarufu wa "Bones," uliokuwepo kwenye Mercury Act 2, hivi karibuni ulishika nafasi ya kwanza kwenye Alternative Radio na kubaki kwenye Global Top 50 ya Spotify. Ushirikiano wa bendi hiyo na rapa kutoka Atlanta Mashariki J.I.D, "Enemy," umekusanya mabilioni ya streams kimataifa na kufikia #6 kwenye chati ya IFPI Global Singles kwa mwaka 2022. Wakiwa wanatawala kucheza kwenye Redio, bado wamesalia kuwa’’ moja ya bendi nne pekee kwa mfululizo nyimbo zao kufika Top 5 ya Alternative radio." Wameshirikiana na wasanii wengi kuanzia Kendrick Lamar, Lil Wayne, na Wiz Khalifa hadi Avicii na mtunzi wa filamu Hans Zimmer. Kama sehemu ya kurudisha kwa jamii, Imagine Dragons wamechangisha mamilioni ya pesa kwa sababu mbalimbali, ikiwa ni pamoja na kupitia shirika lao la kutoa misaada kwa watoto wenye kansa linaloitwa Tyler Robinson Foundation, na lile la kiongozi wao Dan Reynolds' LOVELOUD Foundation pia wamekuwa na tamasha la kusaidia kusaidia vijana wa LGBTQ+. mwaka 2022, Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky aliwataja kuwa mabalozi wa UNITED 24, ambayo inawezesha misaada ya kibinadamu nchini Ukraine. Hivi karibuni, Imagine Dragons ilipendekezwa katika vipengele vinne kwenye tuzo za American Music Awards ikiwa ni pamoja na kipengele cha kundi bora la mwaka, Msanii bora wa Rock, Albamu bora ya Rock na wimbo bora wa Rock." Bendi hiyo pia iliteuliwa kwa "Kundi bora la 2022" kwenye tuzo za People’s Choice Awards kwa mwaka 2022.