Sam Smith

Sam Smith ni msanii na mtunzi wa nyimbo ambaye amefika mauzo ya platinamu mara nyingi, na mshindi wa tuzo za GRAMMY®, BRIT Awards, Golden Globe na Oscars, ni mmoja wa wasanii wa muziki mashuhuri zaidi kutokea katika historia ya muziki kwa siku za hivi karibuni, na amejikusanyia mafanikio yasio na kipimo. 'Gloria' ni albamu ya nne kuitoa ambayo ilipata mafanikio kama ilivyokuwa albamu iliyotangulia  'Love Goes' iliyotoka mwaka 2020. Sam Smith ana mauzo ya albamu milioni 38, mauzo ya single milioni 283 na kusikilizwa mtandaoni kwa zaidi ya mara bilioni 51. Albamu yake ya kwanza "In the Lonely Hour",  ilipata mauzo ya platinum mara kadhaa, ikawa albamu ya kwanza iliyouzwa zaidi katika muongo. Sam na sauti yake ya kipekee, ameshirikiana na wasanii kama vile Calvin Harris kwenye kibao cha kimataifa cha "Promises", Normanni na wimbo unaopendwa wa R&B "Dancing With A Stranger" na supastaa kutoka Afrika Burna Boy kwenye wimbo "My Oasis". Sam Smith anashikilia Rekodi mbili za Dunia za Guinness: moja wapo ni kukaa kwenye chati  ya UK Top 10 Album kwa wiki nyingi mfululizo (kupitia albamu yake ya kwanza ya mwaka 2014, "In The Lonely Hour") na kuwa na wimbo wa kwanza wa James Bond uliofika namba moja kwenye chati za Uingereza (kupitia ushindi wa Oscar  na Golden Globe “Writing’s on the Wall”).