Lollapalooza Paris (France)
Tamasha la kwanza la Lolla Paris lilifanyika mwaka 2017, likibeba wakali kama Red Hot Chili Peppers, The Weeknd, Imagine Dragons, Lana Del Rey, na wengine wengi na ambao waliwasha cheche kwenye moja jiji lililojaa mahaba na mvuto wa kipekee. Tamasha hili limejihakikishia kuwa na listi ya burudani tofauti kila mwaka, hili ni moja ya tamasha ambalo mashabiki hawapaswi kokosa.